MWAKIBETE WAPATA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA, SPIKA TULIA AISHUKURU SERIKALI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson amezindua gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mwakibete, jijini Mbeya.
Uzinduzi huo uliofanyika leo Aprili 19,2025 unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wakati kwa wakazi wa jiji hilo.
Dk. Tulia amewashukuru viongozi wa Serikali kwa kuendelea kupeleka huduma muhimu kwa wananchi, huku akiwataka wakazi wa Jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kumpigia kura kwa kishindo Dk. Samia Suluhu Hassan kama ishara ya kutambua na kuunga mkono kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuboresha maisha ya Watanzania

