JOKATE AONGOZA MATEMBEZI YA VIJANA WAPIGAKURA WA DK. SAMIA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo ameongoza matembezi ya vijana ambao pia ni wapigakura wapya wa Dk. Samia Suluhu Hassan kuelekea katika uzinduzi wa programu hiyo uliofanyika Katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Jokate ameongeza matembezi ya vijana hao leo Aprili 19, 2025 jijini Dar es Salaam wakielekea katika uzinduzi wa programu maalumu ya vijana kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu ambapo jumuiya hiyo imeweka mikakati mbalimbali itakayofanikisha ushindi wa Dk.Samia kupitia kundi la vijana wa Tanzania.

#Kazinaututunasongambele



Powered by Blogger.