TMA YATABIRI MVUA KUBWA PASAKA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua kubwa siku ya Aprili 20,2025 kwenye mikoa minane.

Utabiri huo wa TMA uliotolewa leo Aprili 19,2025 unaonyesha mvua hizo zitanyesha katika maeneo machache ya Mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Dar es salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka hiyo imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.



Powered by Blogger.