KISHINDO CHA RAIS SAMIA MKOANI TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa Muheza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Jitegemee katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizindua usambazaji wa nishati safi ya kupikia kwa Mkoa wa Tanga katika viwanja vya CCM Jitegemee kabla ya kuwahutubia wananchi wa Muheza mkoani humo tarehe 27 Februari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kiwanda cha Chokaa na Saruji cha Maweni Limestone katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda hicho mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Magila ya Muheza, Ester George Barua, ambaye alimruhusu akalie kiti chake cha Rais kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Jitegemee Wilayani Muheza mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025. Rais Dkt. Samia alifurahishwa na mwanafunzi huyo wakati akielezea mafaniko ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Lugha ya Kingereza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Tanga- Horohoro, wilayani Mkinga mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025.
Shamrashamra za wananchi wa Muheza ambao walihudhuria mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uwanja wa CCM Jitegemee Muheza mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025.

Powered by Blogger.