SERIKALI YAWATOA HOFU WANANCHI MSIMAMO WA TRUMP

Na Nora Damian, The Page

Waziri wa Afya, Jenister Mhagama amewataka Watanzania kuondoa hofu kuhusu upatikanaji wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi kwa kuwa wanaendelea kufuatilia na kuhakikisha usalama wa afya za Watanzania unakuwa imara.

Ametoa kauli hiyo leo Januari 30,2025 jijini Dar es Salaam kufuatia msimamo uliotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, wa kusitisha msaada wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi kwa mataifa ya Afrika.

Amesema shughuli zote zinazohusiana na masuala ya afya tunaendelea kuzisimamia kwa kufuata miongozo tuliyonayo, kanuni, sheria na taratibu zetu na tutaendelea kuhakikisha kwamba wananchi wako salama

"Watanzania watulie shughuli zote zinazohusiana na masuala ya afya tunaendelea kuzisimamia kwa kufuata miongozo tuliyonayo, kanuni, sheria na taratibu zetu na tutaendelea kuhakikisha kwamba wananchi wako salama," amesema Waziri Mhagama.

Hivi karibuni Rais Trump aliagiza kusitishwa usambazaji wa dawa za Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu kwa nchi zinazopewa misaada na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID).

Powered by Blogger.