TANZANIA, PAKISTAN KUPANUA WIGO WA USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo (kushoto), akimpatia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Muhammad Ishaq Dar, Kitabu picha kinachoonesha historia ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na Mwandishi Maalumu, Apia Samoa

Tanzania na Pakistan zimekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano ili kukuza uhusiano baina ya nchi hizo huku wakizingatia vipaumbele vya nchi zote kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Wakizungumza pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Muhammad Ishaq Dar, wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika kilimo, teknolojia, viwanda vya nguo na biashara.

Waziri Kombo ameishukuru Pakistan kwa ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania kwa miaka 60 sasa na kumpatia Waziri Dar Kitabu picha kinachoonesha historia ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Photographic Journey: 60 Years of the United Republic of Tanzania) ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameandika dibaji ya kitabu hicho.



Powered by Blogger.