WALIMU WAPEWA MBINU KUFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WAO
Na Mwandishi Wetu, The Page
Mwalimu mkongwe aliyewahi kufundisha viongozi mbalimbali nchini, Maria Kamm amewataka walimu kuwa na uhusiano mzuri na wanafunzi ili kuwawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Kamm ambaye amefundisha viongozi mbalimbali akiwemo Dk. Asharose Migiro ameyasema hayo Septemba 3,2024 wakati wa mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana John the Baptist yaliyofanyika Bunju jijini Dar es Salaam.
“Walimu mnapaswa kujua namna ya kuishi na wanafunzi, mfano mwalimu ukipenda sana kuchapa wanafunzi tambua heshima yako lazima itashuka, kuna haja kubwa ya kuwepo kwa upendo baina ya mwanafunzi na mwanafunzi na walimu na wanafunzi," amesema Mwalimu Kamm.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Siraji Said, amesema mafanikio ya shule hiyo yamechangiwa na ushirikiano uliopo baina ya walimu na wanafunzi hatua iliyowezesha kufanya vizuri katika mitihani ya taifa.
“Matokeo yetu mazuri tunayoyapata ni mikakati mizuri tuliyojiwekea ya kufundisha hasa madarasa ya mitihani, tunamaliza mapema mitaala na kufanya mitihani mingi kwa mfumo ule ule wa mitihani yao mwisho," amesema Mwalimu Said.
Kwa upande wao wahitimu wa kidato cha nne wamewashukuru walimu kwa malezi mazuri waliyowapatia na kuwaasa wanafunzi wenzao kujituma na kuongeza bidii kwenye masomo.
“Matarajio yetu ni kufaulu kutokana na maandalizi mazuri tuliyopatiwa na walimu wetu kwa miaka yote minne, tunawasihi wanafunzi wenzetu wliobaki kuongeza bidii katika masomo yao," amesema mwanafunzi Abigael kwa niaba ya wenzake.