MAMA KANUMBA AGUSWA DUA YA KUWAOMBEA WASANII AKIMKUMBUKA MWANAWE

Mama mzazi wa Steven Kanumba, Frorah Myegoa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa dua ya kuwaombea wasanii na wanamichezo waliotangulia mbele ya haki kwenye viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.


Mwandishi Wetu, The Page

Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu Tanzania, Steven Kanumba, amesema tukio la kuwaenzi wasanii waliofariki dunia limempa faraja kubwa hasa wakati huu wa miaka 12 ya kifo cha mwanawe Kanumba.

Mama huyo Florah Myegoa ambaye pia amempoteza Seth mdogo wa Kanumba, amesema kwa miaka mingi wasanii hawajawa na tukio la kuwakumbuka wenzao waliofariki.

Ameyasema hayo leo Septemba 4,2024 wakati wa dua maalumu ya kuwakumbuka wasanii, wanamichezo na watangazaji nyota waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Suzana Lewis maarufu Natasha.

Florah amesema dua hiyo inamfanya amkumbuke Kanumba kwa kazi nyingi alizozifanya za tasnia ya uigizaji ambazo zilikuwa zinafundisha jamii.

"Nimempata faraja kubwa kwa kuandaliwa kwa jambo hili la kuwaenzi wenzetu waliotangulia mbele za haki, namshukuru Steve Nyerere kuandaa," amesema Frorah.

Naye Suzana Lewis maarufu Natasha amesema waliotangulia mbele ya haki wameacha mapengo mengi ambayo hayawezi kuzibika kutokana na kazi walizozifanya ambazo zimegusa jamii.

"Tutaendelea kuwakumbuka kwa kazi walizozifanya, kuwaenzi ni jambo kubwa sana kulingana na vitu walivyofanya," amesema Natasha.

Amesema baadhi ya wasanii wameondoka wakiwa wangali na umri mdogo na wengine wakubwa alikuwa akishirikiana nao kwa karibu ambao wameacha pengo kubwa.

Amewataja baadhi ya waliotangulia mbele ya haki ambao kazi zao zinaigusa jamii kuwa ni Kanumba, Maunda Zoro na Amina Chifupa ambaye alikuwa rafiki yake na kuwaasa wasanii waliobaki kutumia vipaji vyao vizuri ili waweze kuacha alama.
Powered by Blogger.