WATOTO WA MAUNDA ZORO WAMLIZA MONALISA
Na Mwandishi Wetu, The Page
Msanii Ivone Shell maarufu Monalisa ameangua kilio wakati akiwatambulisha watoto wa marehemu Maunda Zorro kwenye shughuli ya kuwakumbuka wasanii mbalimbali waliotangulia mbele ya haki.
Dua hiyo ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki imefanyika leo Septemba 7,2024 kwenye viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
Monalisa amesema watoto wa Maunda Zorro wamemkumbusha mbali kutokana na urafiki waliokuwa nao huku akisema zaidi ya wasanii 250 walishatangulia mbele ya haki.
"Nawaona watoto wa rafiki na ndugu yangu Maunda Zorro (anaangua kilio)....Mungu awabariki walioandaa jambo hili na huu ni mwanzo litaendelea, hadi sasa idadi ya wasanii wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki ni zaidi ya 250 na tutaendelea kuondoka, hatujui nani baada ya hapa atafuata," amesema Monalisa.
Naye Msanii wa tasnia ya filamu nchini, Chuchu Hansi, amesema ni jambo la busara kuwakumbuka wasanii ambao wametangulia mbele ya haki na kuendeleza mazuri yao.
Amesema katika kuenzi mazuri ya wasanii waliofariki dunia ameshirikisha baadhi ya wasanii waliopo kwenye Kituo cha Sanaa cha Mzee Majuto kilichopo mkoaniTanga.
"Wapo baadhi ya wasanii ambao nimewashirikisha kutoka kwenye Kituo cha Mzee Majuto na muda si mrefu mtaanza kuwaona pindi filamu itakapoanza kuoneshwa katika kituo cha luninga nilikoipeleka," amesema Hansi.