WAZALISHAJI NAFAKA WAHIMIZWA KUONGEZA VIRUTUBISHI KWENYE VYAKULA
Na Nora Damian, The Page
Ili kuondokana na udumavu kwa watoto na vifo vya kinamama walio katika umri wa uzazi Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imesema wasagishaji wote wanapaswa kuongeza virtubishi kwenye unga, mafuta ya kula na chumvi.
Akizungumza Agosti 7,2024 kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayoendelea kitaifa jijini Dodoma, Ofisa Utafiti kutoka TFNC, Francis Milinga, amesema tayari serikali imepitisha sheria ambayo inaelekeza wasagishaji wakubwa kuongeza virutubishi kwenye unga, mafuta ya kula na chumvi.
“Vyakula ambavyo vinaliwa kwa wingi ndiyo vinaongezwa virutubishi, kwenye unga wa ngano na mahindi tunaweka Vitamin B 12, asidi ya folic, madini chum ana zink, kwenye mafuta ya kula tunaweka Vitamin A na kwenye chumvi tunaongeza madini joto. Kwahiyo kanuni imeshapitishwa wasagishaji wote na wengine wale wadogo waongeze virutubishi kwenye vyakula.
“Tukishawashauri tunachukua sampuli kuona kwamba wanaongeza virutubishi, tunashirikiana na Shirika la Viwango TBS na maofisa lishe katika halmashauri mbalimbali kukagua sampuli kama zimeongezwa virutubishi,” amesema Milinga.
Amesema wanayo maabara ambayo inatumika kufanya vipimo mbalimbali kama vile viashiria lishe na virutubishi na kufanya tafiti kwa makundi yaliyo katika hatari ya kupata athari kutokana na lishe.
Taasisi hiyo pia inaratibu uchafuzi wa vyakula kwani vinaweza kusababisha vifo kama vile sumu kuvu kwa kuwashauri watu kufuata kanuni bora za kilimo, uzalishaji na uhifadhi.
Amesema tayari kiwanda cha kutengeneza virutubishi kimefunguliwa Mikocheni na kusisitiza kila mwenye mashine awe na kinyunyizi cha virutubishi.