RAIS SAMIA ATAKA HADHI IREJESHWE SEKTA YA USHIRIKA
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wananchi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Kilimo kuhakikisha inajenga vyama vya ushirika vilivyo imara ili mageuzi yanayofanywa kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi yalete matokeo mazuri.
Rais Samia ameyasema hayo Agosti 8,2024 wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi iliyofanyika katika viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma.
Amesema pia hivi karibuni atakutana na maofisa ushirika nchini ili maono aliyonayo katika kuendeleza sekta hiyo muhimu nchini.
“Ili mageuzi makubwa tunayoyafanya kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi yalete matokeo ya uchumi endelevu ni lazima tujenge vyama vya ushirika vilivyo imara, naitaka Wizara ya Kilimo itupie jicho sekta hii ili kurejesha hadhi na mchango wa ushirika nchini…natafuta siku nikutane na maofisa ushirika nikae nao tuelewane kwa karibu zaidi,” amesema Rais Samia.
Na Nora Damian, The Page