WAKAZI DODOMA WAELEZA SABABU KUJITOKEZA UPIMAJI BURE WA AFYA NANENANE
Na Nora Damian, The Page
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma na maeneo mengine ya jirani wamejitokeza katika upimaji bure wa wa magonjwa yasiyoambukiza na yale yanayoambukiza unaofanywa na Wizara ya Afya kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini humo.
Wizara ya Afya inatoa huduma za upimaji wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, uzazi wa mpango pamoja na huduma za chanjo ya homa ya ini, Covid 19 na chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa mabinti.
Wakizungumza Agosti 6,2024 wameipongeza Wizara ya Afya kutoa huduma hizo kwa kuwa zitawawezesha kutambua hali zao za kiafya.
“Tunaishukuru wizara kwa kutuletea huduma hizi, mimi lilikuja kutembelea maonesho nilidhani kuna vitu vya kilimo na mifugo tu lakini nimepita banda la Wizara ya Afya nikakuta wanatoa huduma za kupima na matibabu nikavutiwa kuja kuchunguzwa afya yangu,” amesema Angel Samson mkazi wa Kikuyu.
Naye Ramadhan Said amesema amesema huduma hiyo inasaidia wananchi kutambua hali zao na kwamba amefurahia kukutana na madaktari na kupatiwa tiba.
Moses Mwalukuta amesema, “Nimepimwa magonjwa tofauti namshukuru Mungu niko salama, tunaomba taasisi nyingine za afya ziige mfano huu yakitokea maonesho kama haya watuletee huduma za afya.
Mratibu wa Mabadiliko ya Tabia katika Jamii kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga, Grace Msemwa, amesema tangu maonesho hayo yaanze wamehudumia watu zaidi ya 1,000 kwa kuwapatia elimu ya masuala mbalimbali ya afya na kuwafanyia uchunguzi wa kiafya.

“Tuna dawati maalumu la uelimishaji masuala mbalimbali ya afya, tunaelimisha kuhusu lishe, maralia, kifua kikuu na dawa asili. Tuna wataalam wa saikolojia yaani afya ya akili na tunafanya uchunguzi na kutoa elimu kuhusu afya ya akili…huduma zote hizi ni bure hivyo, watu wakaribie tuwahudumie,” amesema Msemwa.