VIONGOZI WA DINI WAHIMIZWA KUSIMAMIA UPENDO, AMANI
Taasisi ya Sambaza Upendo, Amani na Umoja imesema imewataka viongozi wa dini kuacha uchonganishi na badala yake wahamasishe upendo, amani na umoja.
Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kamel, Banzai Suleiman, amezungumza hayo alipotembelea makao makuu ya Msikiti wa Shia Kigogo (TIC) walipokuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa makundi maalumu wakiwemo wazee, wajane na watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Banzai amesema viongozi wa dini watakaochonganisha upendo, amani na umoja wa Watanzania watafichuliwa kwa maombi na watatajwa moja kwa moja.
Banzai amesema wapo viongozi wa dini wanaokwenda kinyume na mafundisho ya Mungu ili Watanzania wakose upendo, amani na umoja.
"Tutawafichua viongozi wa dini kwa maombi na kuwataja moja kwa moja kwa sababu kama Mungu ametufikishia tunu ya upendo, amani na umoja wewe ni nani unatutenganisha," amesema Banzai.
Amesema viongozi wa dini wanatakiwa kuwaambia watu namna ya kuliheshimu Taifa kwa kuzingatia misingi iliyokuwepo katika nchi ya upendo, amani na umoja.
Amesema hawawezi kukubali upendo na amani ya nchi uharibike kwa kuwa ni Tanzania pekee unaweza kukuta mchungaji anakwenda msikitini au viongozi wa msikiti wanaenda kanisani bila ya kuogopa.
Naye mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya TIC, Sheikh Mohamed Abdi, amesema kila mtu anapaswa kuishi kwa amani na upendo.
Pia amesema kufanya mambo mema pamoja na kuwaonea huruma viumbe wa Mungu ni mambo yanayompendeza Mungu.
"Mtume wetu Muhammad (saw) hajasifiwa kwa kusali bali alisifiwa kwa kuwasaidia watu waliomzunguka na wenye itikadi mbalimbali ikiwemo waislamu na wakristo pamoja na wasiokuwa na dini," amesema sheikh Abdi.
Sheikh Abdi amesema umoja wa taasisi hiyo ni kioo kwa jamii katika kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu, wajane, yatima yanapaswa kuigwa na kila mmoja.
Kwa upande wake Askofu Mary Mudirikati amesema mbali na kusaidia makundi ya wahitaji wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhitaji wa eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha watoto, sehemu ya kufungua viwanda vidogo na usafiri wa kuwafikia na kueneza upendo na amani ndani ya jamii.