FCC YAWAITA WAKULIMA, WAFUGAJI KUPATA ELIMU YA PEMBEJEO BANDIA
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Na Nora Damian, The Page
Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) imewataka wakulima na wafugaji kununua pembejeo halisi kwenye vyanzo vinavyoeleweka ili kutokomeza bidhaa bandia.
Tume hiyo inatumia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma wanazozitoa kuhakikisha wanamlinda mlaji.
Akizungumza Agosti 5,2024 na waandishi wa habari katika banda la tume hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, amewataka wakulima na wafugaji kufika katika maonesho hayo kujifunza jinsi tume hiyo inavyofanya kazi hasa katika kuwalinda dhidi ya bidhaa bandia.
"Katika kilimo kuna matumizi ya pembejeo hivyo, ni muhimu wakulima wakatumia fursa ya maonesho haya kuja na kupata elimu kuhusu pembejeo feki. Tunatoa elimu pia kwa wavuvi wajue watapataje nyavu sahihi na vifungashio viwe vinavyokidhi viwango," amesema Erio.
Aidha amesema wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango vya ubora kwa kuwa ni muhimu katika ushindani.
Mkurugenzi huyo pia amewataka wakulima na wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuwachagua viongozi wenye maono kama kaulimbiu ya Maonesho ya mwaka huu inavyosisitiza.
"Mchague viongozi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko na wanaoweza kusaidia kufanikisha ushirikiano wa kibiashara, kupata ruzuku na rasilimali nyingine za maendeleo," amesema Erio.
Kaulimbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu inasema; 'Chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo na mifugo'.