TARURA, WAKANDARASI WASAINI MIKATABA GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 24 baina ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na wakandarasi yenye thamani ya Sh bilioni 9.6.
Katika hafla hiyo Shigela amewataka wakandarasi kukamilisha miradi mapema na kwa viwango vyenye ubora ili kuendelea kutengeneza uaminifu kwa serikali na kupewa kazi nyingine.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita, Mhandisi David Msechu, amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Sh bilioni 20.3 zimeidhinishwa na serikali kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara mkoani humo.