FCS KUZINDUA DIRA YA TAIFA KUPAZA SAUTI ZA WANANCHI
Mkurugenzi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Foundation for Civil Society (FCS), Justice Rutenge, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Azaki.
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Foundation for Civil Society (FCS) imesema mwaka 2025 wanatarajia kuzindua Dira ya Taifa ya mwaka 2050 kwa lengo la kupaza sauti za wananchi.
Akizungumza leo Agosti 23,2024 Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Justice Rutenge, amesema dira hiyo itatoa fursa kwa wananchi kupaza sauti zao na kuachana na utamaduni uliopo ambapo wataalamu wamekuwa wakiandika mawazo yao.
Amesema walianza na dira ya Taifa ambayo inaishia mwaka 2025 na sasa wanatarajia kuzindua dira iitakayoishia mwaka 2050 ambayo itakuwa fursa kwa wananchi kupaza sauti zao.
Na Mwandishi Wetu, The Page

"Hii dira tutakayoizindua mwakani ambayo ni fursa inakuja mara baada ya miongo mitatu katika kuandaa dira ya Taifa nyingine, tunalinganisha na nchi nyingine kutengeneza. Inapaswa itokane na sauti, mawazo, mitazamo na maoni ya wananchi ndiyo maana tunasema sauti ni kipengele kwenye kaulimbiu ya Wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) ambayo inatarajiwa kufanyika mkoani Arusha," amesema Rutenge.
Rutenge amesema ifike wakati wakubaliane kuhusu maoni ya Watanzania kuhusu dira hiyo na kuwa pamoja tofauti za kidini, umri na kijinsia mwisho wanakuwa kitu kimoja.
Amesema thamani ya maono yao waliyojiwekea kama Taifa hivyo Wiki ya Azaki watapata ushirikiano kwenye sekta, nyanja na watu wa aina mbalimbali ili kila mtu ashiriki mchakato wa maendeleo.
Pia amesema kulimbiiu ya mwaka huu imejielekeza kwenye kipindi muhimu cha uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Wiki ya Azaki, Nesia Mahenge, amesema katika maadhimisho hayo wataangalia changamoto wanazokutana nazo na vitu gani wanaweza kuvifanya Ili washirikiane pamoja katika sekta zikiwemo za binafsi na wadau wa maendeleo.
"Wiki ya Azaki inaadhimishwa mwaka wa sita, tunajivunia kila mwaka kuendeleza utamaduni huu ambapo Septemba 9 mpaka Septemba 13,2024 tutaadhimisha jijini Arusha," amesema Mahenge.