DIT YAELEZA INAVYOSHIRIKIANA NA VIWANDA KUWAONGEZEA UJUZI WANAFUNZI
Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) imesema wanashirikiana na viwanda mbalimbali ili wanafunzi wapate uzoefu ili wanapomaliza masomo yao waweze kuajiriwa au kujiajiri.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Viwandani Chuo cha DIT, Dk. Sosthenes Karugaba wakati Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) walipokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi wa chuo hicho wanaosoma masomo ya Uhandisi, Sayansi na Teknolojia.
Dk. Karugaba amesema mafunzo ya viwandani yanawajengea mazingira mazuri ambapo wanafunzi hao wanapomaliza na kwenda kuajiriwa au kujiajiri wanafanya kazi kwa ufanisi na kuwa tayari kutumia vifaa vya kisasa.
"Kampuni ya CCCC wamekuja kukutana na wanafunzi wa DIT wanaomaliza mwaka huu ili wawaeleze shughuli wanazozifanya pamoja na fursa zilizopo katika miradi yao mbalimbali wanayoifanya hapa nchini," amesema Dk. Karugaba.
Amesema DIT imekuwa ikiwezesha wanafunzi kupata mafunzo viwandani ambayo husaidia walengwa kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuwa tayari kutumia vifaa vya kisasa.
Naye Naibu Meneja wa CCCC, Liyuliang Lee, amesema wametoa mafunzo kwa wanafunzi hao ili kuwajengea uwezo waweze kujua fursa mbalimbali zilizopo kwenye miradi mikubwa iliyopo ndani na nje ya nchi.

Yee amesema kampuni hiyo inajihusisha na ujenzi ambapo imekuwa ikiwafikia wahitimu katika vyuo mbalimbali ili kufundisha fursa zinazopatika pindi wanapotafuta ajira waweze kujua.
Amesema CCCC imekutana na wanafunzi hao ili kuwapa mafunzo yenye tija ambapo baada ya miaka ijayo watakuwa na viwango vikubwa katika kuchangia uzalishaji wa nchi na kujiongezea kipato.
"Kampuni ya CCCC inamilikiwa na serikali ya China iko nchini Tanzania tangu mwaka 2009 na imekuwa ikijishughulisha na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo," amesema Yee.