FAHAMU SEKTA 13 MUHIMU MAFUNZO YA VETA
Na Nora Damian, The Page
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo yamejikita katika sekta 13 zinazomwezesha kijana kupata ujuzi wa kujiajiri au kuajiriwa.
Veta inatumia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma kunadi sekta hizo kwa lengo la kuongeza uelewa kwa umma na kuhamasisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kusoma.
Akizungumza Agosti 3,2024 kwenye maonesho hayo Ofisa Mkuza Mitaala wa Veta, Anna Nyoni, amesema wanatoa mafunzo katika fani 89 ambazo zimejikita katika sekta tofauti 13.
Amezitaja sekta hizo kuwa ni utalii, sanaa za maonesho na mikono, ufundi vyuma, ufundi umeme, ususi na urembo, kilimo na usindikaji wa vyakula, uchapaji, huduma za biashara, ufundi magari na uziduaji madini.
"Tuna sekta ya kilimo na usindikaji wa chakula na ndiyo hasa ambayo tunaitangaza hapa Nanenane, tuna fani mbalimbali ambazo ni kilimo cha mbogamboga na matunda, fani ya uchakataji wa miti, kilimo cha mazao ya nafaka, 'Bioenergy' na fani ya utunzaji wa mifugo.
"Kwenye utunzaji wa mifugo tunasema kila kinachotoka sisi tunakitumia, kwa mfano kinyesi cha ng'ombe tunakibadilisha kinaweza kutumika kwenye kupikia na shughuli zingine mbalimbali. Pia tuna fani ya kuchakata nyama, fani ya kufuga nyuki pamoja na fani nyingi ambazo zinahusiana na masuala ya kilimo," amesema Nyoni.

Ofisa huyo amesema wanatoa mafunzo katika kozi za muda mrefu na muda mfupi, kozi za muda mfupi zinaanzia mwezi mmoja mpaka miezi sita na za muda mrefu ni kwa miaka mitatu.
"Mwanafunzi anasoma mpaka miaka mitatu ambapo kuna ngazi ya kwanza hadi ya tatu na akifika ngazi ya pili anafanya mtihani wa kitaifa. Tunampa cheti cha ngazi ya pili na akifika ngazi ya tatu pia anafanya mtihani wa kitaifa tunampa cheti cha ngazi ya tatu," amesema.
Ametoa wito kwa Watanzania kuwapeleka watoto wao kusoma Veta ili wajifunze fani mbalimbali kwani wana vyuo 80 na wana mpango wa kuongeza vingine 65 mwakani.