DASPA YASHAURI WAKULIMA WALIOPATA MAFUNZO WAZALISHE MBEGU KWA WINGI KUKIDHI MAHITAJI
Na Nora Damian, The Page
Shirika la Uzalishaji Mbegu Dodoma (DASPA) limeanza kutoa mafunzo kwa wakulima waweze kuzalishaji mbegu za mazao mbalimbali hasa yanayolimwa mkoani humo ili kuhakikisha zinapatikana kwa wingi na kuongeza uzalishaji wa nafaka.
Akizungumza Agosti 3,2024 na Waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa DASPA, Aithan Chaula, amesema shirika hilo linahakikisha mkulima anazalisha mbegu ambazo zitapatikana kirahisi na kwa bei nafuu.
Amesema mpaka sasa wamewafundisha wakulima 45 katika Wilaya ya Chamwino na kwamba wana mpango wa kwenda katika Wilaya za Gairo, Kongwa, Singida Vijijini na Isimani Iringa kwa sababu maeneo hayo yana hali ya hewa kama ya Dodoma.
“Tumejikita katika kuzalisha mazao matano; karanga, mtama, kunde, mbaazi na uwele ambayo tunahakikisha wakulima wanayalima kwa lengo la kupata kipato na chakula. Tunataka wakulima wawe wazalishaji wa mbegu na kuwauzia wenzao ili tuweze kufika sehemu mkulima awe na mbegu za kutosha na uzalishaji wa nafaka uongezeke waweze kutengeneza lishe bora katika ngazi ya kaya na kuwa na kipato,” amesema Chaula.
Kuhusu mbegu ya Mbaazi (Ilonga m 2) amesema inastawi vizuri katika Mkoa wa Dodoma na mkulima anaweza kuanza kuvuna kuanzia mwezi wa sita mpaka wa 12 kisha ataendelea mwaka wa pili bila kupanda zingine, pia inaongeza rutuba kwenye udongo.
“Mfano mwaka huu kilo moja ya mbaazi ni Sh 3,000 hivyo, kipato kitaongezeka kama wakulima wataweza kuzalisha kwa wingi mbaazi,” amesema.
Akizungumzia kunde amesema mbegu waliyozalisha inaweza kulimwa wakati wowote hata wa kiangazi endepo itamwgiliwa au masika na inafanya vizuri zaidi wakati ambapo hakuna mvua nyingi, inarutubisha udongo na haina magonjwa mengi.

Kwa upande wa mtama amesema mbegu waliyozalisha hailiwi na ndege na kwamba zao hilo lina faida mwilini na linaweza kumsaidia mkulima kuongeza kipato.
Kuhusu zao la uwele amesema unastawi katika maeneo ya Dodoma na kwamba lina viini lishe ambavyo vinaboresha afya ya uzazi hasa kwa wanawake kutokana na madini ya ‘silicon’ yaliyomo ndani yake.
Mkurugenzi huyo amesema mbegu za karanga ni zile zenye ukinzani wa mabadiliko ya tabianchi, magonjwa na hali ya hewa yenye mvua kiasi ambazo zina mafuta mengi na lishe ya kutosha na kwamba wanawafundisha wakulima namna ya kuongeza thamani ya zao hilo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kama siagi ya karanga (peanut butter)
“Haya ni mazao ya kimkakati na tunahakikisha tunawafundisha wakulima wawe wazalishaji wa mbegu, tumejikita katika maeneo kame ili kuhakikisha kwamba wanazalisha mazao haya ili waweze kupata lishe na kipato kwa jamii zao,” amesema Chaula.