WANAOTAKA KURUSHA NDEGE NYUKI LAZIMA WAPATE VIBALI, LESENI
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari, akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo baada ya kutembelea Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane viwanja vya Nzunguni jijini Dodoma.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema ndege nyuki ‘drones’ siyo kamera na kusisitiza wanaotaka kurusha kupata vibali na leseni kwa sababu ikifyonzwa na ndege za abiria inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo ajali.
Mamlaka hiyo inasimamia sekta ya usafiri wa anga kuhakikisha usafiri unakuwa salama na watu wanaohusika yaani marubani, wahandisi na wale wanaotaka kuanzisha chuo cha mafunzo au shirika la ndege wana sifa stahiki.
Akizungumza Agosti 5,2024 na Waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, amesema kutokana na teknolojia kukua kumekuwa na utitiri wa ndege nyuki huku wengi wanaozirusha wakiwa hawazingatii sheria, kanuni na taratibu.
Na Nora Damian, The Page

“Ndege nyuki si kamera ni ndege kama zilivyo nyingine, huwezi kuirusha angani bila kutoa taarifa ili sisi tuweze kuwataarifu wana anga wengine kwa sababu ikifyonzwa na ndege zinazobeba abiria inaweza kusababisha madhara makubwa hata ajali kwahiyo, ni lazima upate vibali vya kuendesha, upate leseni, uwe na mafunzo na ujue kanuni za kianga,” amesema Johari.
Mkurugenzi huyo amesema hali ya usafiri wa anga ni nzuri kwa sababu ukaguzi wa mwisho uliofanywa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) walipata alama 69.04 na kwamba wanatarajia kuwa na ukaguzi mwingine hivi karibuni.
“Kuna mapungufu waliyaona lakini kwa sababu tulifanya vizuri walitupa msaada wa fedha Dola milioni moja kupitia Serikali ya China ili tutibu maeneo yaliyokuwa na mapungufu. Mradi tumeukamilisha hivyo watakuja kukagua kuona maboresho tuliyofanya…ni matumaini yetu tutatoka kwenye asilimia 69 na kwenda viwango vya juu zaidi,” amesema.

Kuhusu ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga amesema utagharimu Sh bilioni 78 na tayari Serikali imetenga Sh bilioni 28.2 na wakati wowote watatangaza zabuni ya kimataifa ili kumpata mjenzi.
Mkurugenzi huyo amesema wanatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa umma kuhusu usafiri wa anga, masharti, kanuni na taratibu.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Aristid Kanje, amesema wanatoa mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kurusha ndege nyuki ambapo wanafundisha kuelewa sheria na kanuni za urushaji.
“Tunawaelimisha wananchi hasa wakulima wajue namna bora ya kutumia ndege nyuki katika kuboresha kilimo, unaweza kutumia kufanya ukaguzi wa shamba, kujua sehemu ya kuweka mbolea na kufanya kilimo kikawa rahisi, kwa gharama nafuu na chenye tija,” amesema Kanje.
Amewakaribisha watu mbalimbali kupata mafunzo katika chuo hicho kwa kuwa kinatambuliwa kimataifa na wahitimu wana uwezo wa kupata ajira ndani na nje ya nchi.