WANAFUNZI WAASWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI
Na Mwandishi Wetu, The Page
Wanafunzi nchini wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi kwa kuwa teknolojia inawahitaji wataalamu wanaoweza kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua.
Ofisa Elimu Taaluma wa Halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani, Juma Yusuph, amezungumza hayo wakati Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano inayomilikiwa na Serikali ya China (CCCC) ilipokuwa ikitoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Baobab iliyopo Mapinga wilayani humo.
Yusuph amesema nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na wataalamu wa sayansi wanaoweza kufanya miradi mbalimbali itakayofanikisha kupiga hatua nchi yetu.

“Tunaishukuru Kampuni ya CCCC imesaidia kuleta hamasa katika kuhamasisha vijana wasome masomo ya sayansi na nchi haiwezi kuendelea bila ya kuwa na wataalam.
“Hii inaleta chachu kwa wanafunzi wetu wanaosoma masomo ya Sayansi na ukizingatia maendeleo mengi yanakuja kutokana na ufanisi mkubwa katika tasnia ya uhandisi katika ujenzi, ikiwemo barabara na mawasiliano kwa sababu tupo kwenye mfumo wa teknolojia inahitaji wataaalamu wengi,”amesema Yusuph.
Naibu Meneja wa Kampuni ya CCCC, Li Yuijang, amesema wametoa mafunzo kwa njia ya vitendo ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi ikiwemo upimaji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama madaraja.
“Tumekuja na wahandisi mbalimbali kutoka China wanawafundisha wanafunzi mbinu za ujenzi zitakazowasaidia maisha yao ya baadaye na tunawaonyesha vifaa vinavyotumia katika kutengeneza miundombinu mbalimbali kama ujenzi wa madaraja na barabara,”amesema Yuijang.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Baobab, Venance Wangoha, amesema wameshuhudia kampuni hiyo ikionyesha kazi wanazofanya nchini kuhusiana na uboreshaji wa miundombinu pamoja na kuhamasisha wanafunzi kusoma sayansi.
“Tumeona vifaa wanavyotumia katika kutengeneza miundombinu mbalimbali kwa kutumia mashine zinazohusiana na masomo ya sayansi watoto wamefundishwa na kutiwa moyo,”amesema Wangoha.
Mwanafunzi wa shule hiyo, Amor Bayumi, amesema wamejifunza njia mbalimbali za kutengeneza madaraja ambayo yatapita juu ya bahari na kwenye ardhi iliyopata dhoruba ya kimazingira ikiwemo mpasuko wa ardhi.
Mwanafunzi mwingine wa kidato cha sita, Amrat Haishaul, amesema mafunzo hayo yamewahamasisha kusoma masomo ya sayansi kwa kuwa watakapomaliza masomo yao watapata ajira.