VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KWENYE MIRADI YA KILIMO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Jerald Mweli, akizungumza wakati wa kongamano la vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini lililoandaliwa na Shirika la Mageuzi ya Kijana Tanzania (AGRA) kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT).
Na Mwandishi Wetu, The Page
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Jerald Mweli amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.
Mweli ameyasema hayo katika kongamano la vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini lililoandaliwa na Shirika la Mageuzi ya Kijana Tanzania (AGRA) kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) lililohudhuriwa na vijana 100 kutoka mikoa mbalimbali nchini.
"Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali tumeandaa mpango maalumu kuhakikisha vijana wanajitengenezea ajira ya kudumu kupitia kilimo, sasa hivi International Forum zote zitahusisha vijana ambapo watakuwa wakisafiri nje ya nchi ili wakajifunze namna ya kuwekeza kwenye kilimo," amesema Mweli.
Amesema vijana watakapojiajiri kwenye kilimo kinalipa kwa kuwa baadhi ya mashirika kutoka mataifa ya nje yanataka kuleta fedha kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wanaojihusisha na kilimo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AGRA, Vianey Rweyendela, amesema uchumi wa Tanzania umefikia asilimia 5.1 kwa mwaka kutokana na shughuli za kilimo.
"Kukua kwa uchumi wa nchi kumetokana na kilimo kwani asilimia 65 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo," amesema Rweyendele.
Amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bajeti ya kilimo imeongezeka zaidi ya mara tano tofauti na vipindi vilivyopita lengo likiwa ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Rweyendele amesema AGRA kupitia mradi wa BBT imelenga kuwasaidia vijana wakulima katika upatikanaji wa masoko, mashamba na kuwakopesha fedha ili waweze kufanya shuguli za kilimo.
Mkurugenzi wa Kikomba Avocado Farm, Emmanuel Kisinda, amesema wananufaika na AGRA na wapo katika mafunzo hayo kwa lengo la kujua sera ambazo wanaweza kuona kijana anasaidiwa kwenye upatikanaji wa masoko, fedha na ardhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkame, Mkame Tetere, amesema wana changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo ikiwemo ukosefu wa mbegu kwa wakulima wa vijijini.
"Tunaamini AGRA wakiweka mfumo mzuri wa kuwakopesha wakulima mbegu hakuna atakayewabana wakulima," amesema Mkame.