TMDA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imewataka wananchi kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya dawa kwa kuwa yanachangia usugu katika kupambana na vimelea vya magonjwa.
Akizungumza kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo, amesema usugu wa dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi yasiyo sahihi na kusababisha wananchi wengi kupata madhara.

"Wananchi wazingatie matumizi sahihi ya dawa, waache kutumia dawa kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu, tunaendelea kuelimisha jamii kuhakikisha dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi," amesema Fimbo.
Amesema wanatumia maonesho ya Sabasaba kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kufahamu majukumu ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi huyo ametoa mwito kwa wananchi kutembelea banda la taasisi hiyo kupata elimu sahihi juu ya udhibiti na matumizi sahihi ya dawa na vitenganishi.