JINSI MAHAKAMA YA WATOTO INAVYOFANYA KAZI
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Temeke, Orupa Mtae, akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la mahakama katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Jamii imehimizwa kutambua umuhimu wa mahakama ya watoto ili kuhakikisha haki zao zinalindwa na kupanua wigo wa ulinzi wa watoto.
Akizungumza Julai 8,2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Temeke, Orupa Mtae, amesema mahakama hiyo inasikiliza mashauri yote yanayomuhusu mtoto pale ambapo amekinzana au amekutana na sheria.
Amesema mahakama hiyo inasikiliza mashauri ya madai pale ambapo mtoto atakuwa amefanya kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu
“Kwa mfano mtoto akiiba, akibaka, atalawiti au atafanya kosa lolote lililoainishwa kwenye kanuni ya adhabu sura ya 16 ataletwa katika mahakama ya watoto kupitia polisi. Tunaangalia ustawi bora wa mtoto, pale ambapo analetwa mahakamani tutaangalia hata kama ni mshtakiwa tutahakikisha haki zake za msingi hazivunjwi.
"Mtoto anapokuwa mahakamani sheria inataka awe na mwakilishi wakili wa utetezi kwa ajili ya kumsaidia katika mambo yote ya kisheria, pia atakuwa na mzazi au mlezi wake ili jambo lolote linaloendelea mahakamani kama halielewi amsaidie…tunahakikisha lugha inayotumika ni rahisi na nyepesi,” amesema Hakimu Mkazi, Mtae.
Aidha amesema masuala mengine ya kisheria wanayozingatia ni kwamba mtoto haulizwi maswali ambayo yanaweza kutweza utu wake au kumfanya aogope ili aweze kuona haki inatendeka.
“Tukiona ushahidi umejitosheleza au Jamhuri imefanikiwa kuthibitisha shitaka mtoto atapata nafasi ya kujitetea na baada yah apo hakimu ataandika maamuzi kumtia hatiani au kumuachia huru. Ikitokea ametiwa hatiani kabla ya adhabu mara nyingi huwa tunawapa nafasi maofisa ustawi wa jamii kuandika taarifa ya kiuchunguzi ambayo itatuletea mambo ya ziada ambayo pengine hayakuweza kufahamika mahakamani," amesema.
Amefafanua kuwa zipo adhabu mbadala ambazo zitamwezesha mtoto kuendelea na masomo yake au mzazi kulipa faini, fidia kwa mhanga au mtoto kupelekwa kwenye shule ya maadilisho.
Hakimu huyo amesema pia wanasikiliza mashauri ya matunzo ya mtoto na ulinzi wa mtoto na kusisitiza kuwa wazazi wote wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanatunzwa.
“Wazazi wawili wanaweza kuishi pamoja kisha baada ya muda wakatengana, kukatokea ubishani nani anakaa na mtoto, mmojawapo anaweza kuja mahakamani ili mahakama iamue nani anatakiwa kuishi na mtoto. Tunaposikiliza mashauri haya tunaangalia vigezo mbalimbali ambavyo viko kisheria ikiwemo umri wa mtoto, jinsi, kutomsumbua mtoto na nyingine,” amesema.
“Kuna mazoea ya Kiafrika na Kitanzania kwamba baba akiondoka na mtoto anabeba jukumu lote na mama hajishughulishi na jambo lolote. Kwenye mahakama ya mtoto sheria inasema mwenye jukumu la kulea ama kutunza mtoto ni la mzazi, anaweza akawa baba au mama.
“Kwahiyo hata kama baba ameachiwa mtoto anao wajibu wa kumwambia mama achangie hata kwa sehemu kiasi kitakachosaidia katika malezi na matunzo ya mtoto, hata mama akija mahakamani akisema baba achangie tutamwambia pia kama ana kipato na yeye achangie kiasi fulani.
“Nitoe rai kwa baba ambao wanadhani kwamba jukumu hili ni la kwao peke yao wanaweza kuja mahakamani na mashauri yao kusikilizwa ili mzazi wa kike naye aweze kuchangia,” amesema Hakimu Mkazi, Mtae.
Hata hivyo amesema mashauri kama hayo huanzia kwa maofisa ustawi wa jamii na ikishindikana wahusika huelekezwa kwenda mahakamani.