PURA KUFANYA UTAFITI GESI ASILIA KUWEZESHA UPATIKANAJI NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) imesema inafanya tafiti mbalimbali za gesi asilia nchini ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
Hayo yamesemwa Julai 12,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.
“Kwenye upande wa matumizi ya nishati dunia yote inaongelea nishati safi inayozuia uchafuzi wa mazingira, Tanzania tumeweka malengo ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2034 hivyo, lazima tutoke kwenye matumizi ya nishati ambayo inachafua hali ya hewa ikiwemo mkaa, kuni na nyingine tukatumie nishati ambayo haichafui,” amesema Mhandisi Sangweni.

Amesema wanatekeleza kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu (Tanzania ni mahali sahihi kwa uwekezaji) kwa kujenga mazingira bora na yanayovutia wawekezaji ambao ndio wanaokuja kufanya tafiti katika mkondo wa juu wa petroli.
Amesema katika mnyororo wa kuongeza thamani petroli kuna mkondo wa juu unaohusu kutafuta, kuendeleza na kuzalisha petroli na mkondo wa kati wa kusafisha na kuchakata petroli kupata petroli, dizeli na mafuta ya taa na mengine na mkondo wa chini unaohusika kuuza mafuta baada ya kusafishwa.
“Sisi tunadhibiti shughuli za utafutaji hapa nchini, katika maonesho haya tunaeleza shughuli ambazo tunadhibiti na nini tunakifanya, katika kuendeleza shughuli za utafiti tunategemea mwaka huu mwishoni au mwanzoni mwa mwaka ujao tutatangaza maeneo mbalimbali ambayo tutavutia wawekezaji kwa ajili ya kuja kushirikiana nasi kwenye kutafuta,” amesema.
Amesema kati ya kilomita za mraba 945,000 maeneo yenye viashiria vya kuwepo mafuta nchini ni kilomita za mraba 534,000 ambayo ni karibu asilimia 50 ya eneo lote la Tanzania.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, katika maeneo yenye viashiria hadi sasa tafiti zimefanyika eneo lenye kilomita za raba 160,200 na kwamba wataendelea kutangaza vitalu hivyo kwa awamu.