HUDUMA YA INTANETI MAJUMBANI YAWAVUTIA WENGI SABASABA, 200 WAOMBA KUUNGANISHIWA
Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya TTCL (T Pesa), Lulu Mkudde, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Zaidi ya watu 200 wameomba kuunganishiwa huduma ya intaneti majumbani ambayo haina ukomo inayotolewa na Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL).
Shirika hilo limesema linafungua milango ya kidijitali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania kutumia huduma ya intaneti kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akizungumza leo Julai 12,2024 na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya TTCL (T Pesa), Lulu Mkudde, amesema huduma hiyo 'Fiber mlangoni kwako' inampunguzia mlaji ukali wa gharama za vifurushi vya mara kwa mara.

"Tulikuwa tukisikia kwamba vifurushi vinaisha kwa haraka lakini huduma yetu haina ukomo na wateja wengi wanahitaji... imekuja kuleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifurushi vya kawaida," amesema Mkudde.
Amesema pia katika kuunga mkono kaulimbiu ya maonesho hayo walibuni huduma ya Wi - Fi ya T - Cafe kuwawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kufanya shughuli zao kidijitali hivyo kuleta ufanisi na matokeo chanya.
"Shirika limeanzisha huduma hii kuwawezesha walengwa wote kufanya shughuli zao kwa haraka na kwa gharama nafuu," amesema.
Aidha amesema kupitia huduma ya TTCL Pesa mteja anaweza kufungua bila kuwa na kadi ya simu na kwamba anachopaswa kufanya ni kuipakua na kufanya huduma zote za kifedha.
Kuhusu mkongo wa taifa wa mawasiliano amesema mpaka sasa wameshasambaza katika mikoa yote nchini na wilaya 98 tayari zimefikiwa.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, hivi sasa shirika hilo liko kwenye hatua za kuunganisha mkongo wa taifa wa mawasiliano katika Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC).

Mkurugenzi huyo amesema maonesho ya Sabasaba yamewapa fursa mbalimbali kama vile kuonyesha bidhaa zao na kukutana na wateja na kuwapa elimu.
"Tulihakikisha tunawaeleza wananchi miradi ya kimkakati inayosimamiwa na shirika letu ambayo ni mkongo wa taifa na kutoa mafunzo mbalimbali.
"Tuliwaeleza kuhusu Kituo cha Kutunza Kumbukumbu (Data Centre), huduma za TTCL Pesa ili kuhakikisha Watanzania wote wanafahamu. Tunawahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kwamba huduma hizi ni wezeshi katika utekelezaji wa majukumu yao," amesema Mkudde.