WAFANYABIASHARA WATAKA WAZAWA WAPEWE KIPAUMBELE SOKO LA KARIAKOO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo imeiomba Serikali kuwapa kipaumbele katika Soko la Kimataifa la Kariakoo ili kuepuka kumilikiwa na wageni.
Akizungumza leo Juni 7,2024 na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana, amesema
kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni kutoka mataifa mbalimbali kama vile China hatua iliyosababisha kuwapo kwa ushindani hasa wa bei.
"Tunataka kuwe na sheria ya kuwafanya wazawa waweze kumiliki soko na asilimia kubwa iwe ni wafanyabiashara wa Kariakoo. Asilimia 70 ya maduka yamilikiwe na wafanyabiashara Kariakoo, tukikaa kimya wakiingia wengine wataivuruga Kariakoo," amesema Mbwana.

Wafanyabiashara hao pia wameiomba Serikali kuweka mfumo utakaorahisisha ulipaji kodi mbalimbali katika mwamvuli mmoja ili kuepusha usumbufu kwa wafanyabiashara.
"Hatupendi kuona usumbufu unaofanyika Kariakoo siyo afya kwa wafanyabiashara, masuala yote ya kodi yamalizike bandarini. Leseni za wafanyabiashara zijumuishe tozo za 'fire', taka na nyingine ili wafanyabiashara wawe huru wafanye biashara zao kwa amani," amesema.
Hata hivyo amesema suala la utoaji risiti za kielektroniki (EFD) bado ni changamoto na kushauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutengeneza bandari kavu kubwa ili mizigo mikubwa ithaminishwe kirahisi.
Naye Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Peter Mbilinyi, ameshauri kuwe na ushirikishwaji wa taasisi mbalimbali za serikali kuepuka usumbufu kwa wafanyabiashara na kulinda mitaji yao.
Mjumbe wa jumuiya hiyo, Justin Beda, amependekeza Serikali ichukue hatua dhidi ya wafanyabiashara wasio rasmi wanaofanya biashara mbele ya maduka ya watu ili kunusuru soko hilo.
Jumuiya hiyo pia inatarajia kufanya mkutano na wafanyabiashara Juni 13,2024 jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kwa mustakabali wa Soko la Kariakoo.