RAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA RC SIMIYU
Rais Samia Suluhu Hassan.
Na Mwandishi Wetu, The Page
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda na kumteua Kennan Kihongosi kuwa mkuu wa mkoa huo.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyotolewa leo Juni 11,2024 imesema Rais Samia pia amemteua Elias Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba.Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda.
Wengine walioteuliwa ni Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu ambaye anachukua nafasi ya Dk. Stephen Mwakajumilo na George Herbert kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo Herbert alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.


