MATARAJIO YA TANZANIA ZIARA YA RAIS EMBALO
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samuel Shelukindo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embalo.
Wakati Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embalo akitarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini itakayoanza Juni 21 hadi 23 mwaka huu, Tanzania itanufaika na mambo matano.
Akizungumza leo Juni 20,2024 na waandishi wa habari Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samuel Shelukindo, amesema ziara hiyo inatarajia kuibua maeneo ya ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo ya kilimo.
Ametaja manufaa mengine yanayotarajiwa katika ziara hiyo kuwa ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi, kusaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo na kuinua kiwango cha ufanyaji biashara na uwekezaji.
Na Nora Damian, The Page

“Ziara hii itatoa fursa kwa nchi zote mbili kujadiliana katika masuala mbalimbali ya ushirikiano na uwekezaji katika biashara. Tutasaini makubaliano ya ushirikiano yatakayowezesha misingi ya kuendelea kushirikiana na Gine Bissau,” amesema Dk. Shelukindo.
Kwa mujibu wa Dk. Shelukindo urari wa biashara kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 ulikuwa chini ya Dola 200,000 na kwamba ziara hiyo itasaidia kuinua kiwango cha ufanyaji biashara na uwekezaji hasa kupitia Soko Huru la Afrika (AfCFTA) ambalo Tanzania imeridhia.
Amesema rais huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Marais wa Afrika Wanaopambana na Malaria (ALMA) atatembelea miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) na Eneo Huru la Uwekezaki (EPZA).
Rais Embalo na ujumbe wake wanatarajiwa kuwasili nchini Juni 21 na Juni 22 atapokelewa Ikulu na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo watakuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye mazungumzo rasmi kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Guinea Bissau.