INEC YAWATAKA WATENDAJI KUTUNZA VIFAA
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoani Kigoma kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vitumike maeneo mengine nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa INE, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mafunzo kwa waratibu wa uandikishaji wa mkoa, maafisa waandikishaji, maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo, maafisa uchaguzi, maafisa ugavi na maafisa Tehama wa halmashauri yaliyoanza leo Juni 20 hadi 21,2024 mkoani Kigoma.
“Ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” amesema Jaji Mwambegele.
Amesema kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa kutasababisha athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hilo muhimu na kuwataka kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na tume ili waweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapoanza.
Aidha, Jaji Mwambegele amesema matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.
“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote msisite kuwasiliana na tume,” amesema.

Kabla ya kuanza mafunzo hayo washiriki walikula kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rose Kangwa.
Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapigakura (Voters Registration System - VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
“Mafunzo yanawajengea umahiri wa kuwafundisha maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kisha nao watatoa mafunzo hayo kwa waendeshaji wa vifaa vya bayometriki na waandishi wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” amesema Jaji Mwambegele.
Aidha, Maafisa Tehama watapatiwa mafunzo maalumu ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi (Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele amewaambia watendaji hao kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima na kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Jaji Mwambegele ametoa angalizo kwa mawakala hao kutoka vyama vya siasa kuwa hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.
Uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura utafanyika Julai Mosi,2024 mkoani Kigoma ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kaulimbiu ya uboreshaji inasema; 'Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora'.