GLOBAL LINK KUENDELEA KUFADHILI WANAFUNZI WANAOTAKA KUSOMA IRAN
Na Mwandishi Wetu, The Page
Taasisi ya Global Education Link Ltd imeahidi kuendelea kufadhili wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania kwenda kusoma Iran kwani ni sehemu salama.
Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Asefe Tirabian, ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika maonyesho ya Mama na Binti yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
"Tunahamasisha wanafunzi Tanzania kwenda Iran kupata elimu, hatua hiyo inaleta ushirikiano kati ya Iran na Tanzania.
"Mwitikio wa wanafunzi unaridhisha, nataka kuwaahidi kwamba taasisi hii ni nzuri, imara na Iran ni nchi salama, waliokuwa na utayari na sifa wanakaribishwa kuomba kwenda kusoma kwa ufadhili wa Global," amesema Asefe.

Global Education Link inashirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufadhili wanafunzi wa Tanzania kwenda kusoma Iran.
Mwaka wa masomo 2024/2025 wanafadhili wanafunzi wa elimu ya juu kwa tahasusi ya Sayansi, Biashara na Sanaa.
Mwaka wa masomo 2024/2025 wanafadhili wanafunzi wa elimu ya juu kwa tahasusi ya Sayansi, Biashara na Sanaa.
