DK. MWINYI AGOMA KUONGEZA MUDA WA KUBAKI MADARAKANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi.

Na Mwandishi Wetu, The Page

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar imesema Rais Dk. Hussein Mwinyi anaheshimu utaratibu uliowekwa wa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano.

Kurugenzi hiyo imetoa taarifa hiyo baada ya hivi karibuni kuwepo kwa maoni yanayopendekeza Rais Dk. Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Juni 24,2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilary, imesema jambo hilo halina tija wala faida kwa nchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia na kuwasihi wenye mawazo hayo wafunge mjadala huo.

“Rais Dk. Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na Sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya mheshimiwa Rais wala si ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar,” amesema Hilary.



Powered by Blogger.