SERIKALI YAJIVUNIA MAFANIKIO MUHAS
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, akizungumza wakati wa kongamano la 12 la kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Serikali imesema inajivunia mafanikio yaliyopatikana katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) tangu kilipoanzishwa mwaka 1963 hasa katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu.
Akizungumza leo Juni 27,2024 wakati wa kongamano la 12 la kisayansi la MUHAS, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, amesema chuo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti za afya zenye tija.
Amesema MUHAS kinaongoza katika tafiti nyingi za afya hapa nchini na kimeweza kuleta mapinduzi makubwa kwenye sera na miongozo inayotumika ndani na nje ya nchi katika kuboresha huduma za afya, kutoa matibabu sahihi na kuzuia magonjwa.
“Tafiti zimechangia katika kukiweka chuo katika nafasi nzuri kulinganisha na vyuo vingine duniani, katika tafiti nyingi zinazochapishwa katika majarida yenye hadhi ya juu wengi waliopata tuzo wanatoka Muhas,” amesema Profesa Nombo.
Amesema pia kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kuchumi (Hits) serikali imejenga na kukarabati majengo zaidi ya 130 kote nchini kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji na kwamba inatarajia kujenga Kampasi kubwa ya Muhas mkoani Kigoma ili kuifanya Kampasi ya Mloganzila kuwa mji wa mafunzo ya afya.
Katibu Mkuu huyo amesema serikali inatarajia kujenga awamu ya pili ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu na Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Afya ya Kinywa ili kuwezesha Kampasi ya Mloganzila kuwa kitovu cha mavunzo ya ubobezi ya afya na sayansi shirikishi, tafiti, ubunifu na huduma za kibingwa na bobezi nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki na kukuza utalii tiba.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa, amesema wanajivunia maendeleo yaliyofikiwa hasa katika nyanja za mafunzo na tafiti na kuwa kitovu cha kutegemewa kwa matokeo ya tafiti za afya zinazosaidia sera na miongozo na taasisi nyingine nchini.
Amesema hadi sasa chuo kina miradi ya tafiti 150 ambayo inafadhiliwa na washirika mbalimbali na kwamba wanaweza kuzalisha machapisho kati ya 450 hadi 500 kwa mwaka.
Amesema kongamano hilo linalenga kutafakari maendeleo waliyofikia kupitia tafiti katika kupunguza changamoto za kiafya katika jamii na kujadili njia za kusonga mbele.
Katika kongamano hilo mwanafunzi wa mwaka wa tatu Dk. Edward Mhina, ambaye aliwasilisha utafiti kuhusu matumizi ya dawa wakati wa wajawazito ameishauri Serikali kuweka msisitizo wa kuzuia matumizi ya dawa kiholela ili kuepusha madhara kwani zikitumika kwa muda mrefu husababisha ufubavu.

Kongamano hilo pia limetumika kumuenzi aliyekuwa mkuu wa kwanza wa chuo hicho Hayati Rais Ally Hassan Mwinyi kutambua mchango wake hasa katika upanuaji wa miundombinu ya kufundishia, kutoa huduma na tafiti ikiwemo uanzishwaji wa Kampasi ya Mloganzila.