SAMIA, MARAIS WASTAAFU AFRIKA KUJADILI ULINZI, USALAMA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam.
Na Nora Damian, The Page
Marais wastaafu wa Nigeria, Burundi, Msumbiji na Tanzania wanatarajia kukutana kujadili ulinzi na usalama wa nchi za Afrika wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC - AU).
Marais hao Jakaya Kikwete, Olesegun Obasanjo, Domitien Ndayizeye na Joachim Chissano wataungana na watu wengine mashuhuri katika maadhimisho hayo yatakayofanyika nchini Mei 25,2024 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo.
Akizungumza leo Mei 22,2024 na Waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema baraza hilo lililoanzishwa Mei 25,2004 lina wajumbe 15 kati ya nchi 55 wanachama wa AU wanaoteuliwa kwa mzunguko limekuwa likifanya kazi ya kusuluhisha migogoro inayojitokeza Afrika.
“Kila mwezi kunakuwa na mwenyekiti wa baraza na kwa mwezi huu Tanzania itakuwa mwenyekiti, hii ni heshima kubwa kuadhimisha miaka 20 wakati uenyekiti ukiwa chini ya Tanzania. Tanzania inaongoza katika kusaidia jitihada za kupatikana amani barani Afrika na viongozi wengine wa Tanzania wameshiriki kama wasuluhishi wa migogoro mbalimbali barani Afrika,” amesema Makamba.
Viongozi wengine watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Uganda, Jesca Alupo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Muossa Faki Mahamat.
Machi 2022 Tanzania ilichaguliwa kuhudumu kama mjumbe katika baraza hilo na kufikika kikomo Machi 2024. Hata hivyo imechaguliwa tena kuhudumu katika baraza hilo hadi mwaka 2026.
Baraza hilo ndio chombo cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama Afrika ambapo limekuwa likijishughulisha kutatua migogoro inayojitokeza katika nchi mbalimbali wanachama.