KUNDO ATAKA KASI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew amezielekeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijinini (RUWASA) na Bonde la WAMI/RUVU kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji ili kutimiza azma ya serikali ya upatikanaji maji kwa asilimia 85 vijijini na 95 mjini ifikapo 2025.
Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Morogoro ambapo alikugua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji ikiwemo mradi wa maji wa Mgulu wa ndege, mradi wa maji wa Sokoine ambao aliuwekea jiwe la msingi na mradi wa maji katika Kijiji cha Kichangani ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wananchi.
Kundo alikemea suala la wananchi kutumia maji na mifugo katika eneo moja na badala yake kuwepo na vituo vya kuchotea maji na mabirika maalumu ya kunyweshea mifugo.
“Wananchi wanaoishi katika Manispaa ya Morogoro vijijini ambao ni wakulima na wafugaji ni lazima wanywe majisafi na salama na sio maji yanayotoka kwenye mabwawa ambayo wanachangia na mifugo, hiyo haikubaliki," alisema Kundo.
Aidha aliwataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya miradi ya maji.
“Tabia ya kuharibu miundombinu ya maji sio jambo zuri, kila mwananchi ana wajibu wa kutunza miundombinu hiyo kwasababu inatumia gharama kubwa," alisema.
Aliwataka wataalam wanaohusika na maunganisho ya maji kutumia siku saba kuwaunganishia maji wananchi katika nyumba zao, pia kuwepo kwa ushirikishwaji katika usomaji wa dira za maji ili kuepuka malalamiko.