VICHWA MCHONGOKO VYA SGR VYAWASILI
Vichwa vya kuchongoka vya treni ya umeme ambavyo vimepokelewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) vikiwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepokea seti ya kwanza ya treni iliyoundwa kwa teknolojia ya kisasa (EMU) yenye vichwa vya muundo wa kuchongoka itakayotumika katika reli ya mwendokasi.
Seti hiyo iliyopokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya seti 10 zinazotarajiwa kuwasili na kila moja ina uwezo wa kuchukua mabehewa manane yatakayobeba abiria 589.
Akizungumza leo Aprili 3,2024 wakati wa kupokea seti hiyo Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema imetengenezwa Korea Kusini na Kampuni ya Hyundai Rotem ambayo imebobea katika ujenzi wa vichwa vya reli.
“Tumeagiza seti kumi za vichwa ambavyo vinagharimu Dola milioni 190, reli yetu ya kisasa itatumia sana vichwa vya namna hii hasa kwa masafa mafupi ya kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Dodoma.
“Leo tumepokea seti ya kwanza na kila mwezi tutaendelea kupokea mpaka zitakapokamilika kumi,” amesema Profesa Mbarawa.
Amesema pia vichwa hivyo vina mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa na kwamba vitafanyiwa majaribio ya kiufundi kwa hatua kabla ya uendeshaji wa kubeba abiria.
Meneja Mradi Manunuzi wa vichwa hivyo kutoka TRC, Mhandisi Kelvin Kimario, amesema vina uwezo wa kumuongoza dereva hata kama atang’ang’ania kuzidisha mwendo.
“Kuna maeneo ambayo itabidi ziende kwa mwendo maalumu mfano kwenye maeneo yenye mahandaki kama kule Kilosa huwezi kupita kwa mwendo wa 160.
“Tulizingatia pia watu mwenye mahitaji maalumu, kwenye treni hizi tuna choo ambacho hata mama akienda na mtoto kujisaidia kuna sehemu ya kumuweka mtoto na sehemu ya kubadilisha nguo.
“Tuna vyoo ambavyo watu wenye ulemavu wa miguu wanaweza kuingia na viti vyao wakapata huduma, kwa wasioona pia tulizingatia mahitaji yao kuna maandishi ambayo wanaweza kupapasa na kujua ujumbe uliopo,” amesema Kimario.
Na Nora Damian, The Page

Kaimu Mkurugenzi wa TRC, Amina Lumuli, amesema kazi ya kushusha vichwa hivyo ilianza tangu Aprili Mosi na baada ya kukamilika wataanza kuvifanyia majaribio.
“TRC tuko kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi, tunaendelea na maandalizi kabla ya kuanza uendeshaji rasmi. Mpaka sasa tumeshapokea mabahewa 65 na vichwa tisa vya kawaida vya umeme,” amesema Lumuli.
Mpaka sasa njia ya SGR inapitika kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma na tayari TRC imeanza majaribio ya treni ya mwendokasi na safari kadhaa zimefanyika za kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.