MAKALLA ATEULIWA KATIBU MWENEZI, JOKATE APELEKWA UVCCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla.

Na Nora Damian, The Page
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imemteua Amos Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi Uenezi na Mafunzo huku John Mongella akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
 
Makalla ambaye awali alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anachukua nafasi ya Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha uliokuwa ukiongozwa na Mongella.
 
Wengine ni Ally Hapi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi huku Jokate Mwegelo akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella.

Hapi ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara anachukua nafasi ya Gilbert Kalima aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Jokate alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
 
Mabadiliko hayo madogo ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa yametangazwa leo Aprili 3,2024 baada ya halmashauri kuu kukutana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Machi 31,2024 Rais Samia alifanya mabadiliko madogo ya viongozi wa wizara, mikoa na wilaya yaliyowagusa pia Makalla na Mongela ambao ilielezwa kuwa watapangiwa kazi nyingine.

 



Powered by Blogger.