WAHITIMU KIDATO CHA NNE 2023 RUKHSA KUBADILISHA TAHASUSI, KOZI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohammed Mchengerwa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha tano na vyuo vya Serikali mwaka 2024.
Serikali imeruhusu wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2023 kubadili tahasusi za kidato cha tano na kozi mbalimbali walizochagua ili kutoa nafasi zaidi kusoma zile zitakazowaandaa kuwa na utaalam katika maisha yao ya baadaye.
Wakati wa ujazaji fomu za machaguo ya awali tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha na matokeo hayakuwa yametoka kuwawezesha wahitimu kuwa na machaguo mazuri zaidi kulingana na ufaulu wao.
Akizungumza leo Machi 20,2024 na Waandishi wa habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa, amesema hatua hiyo ni maandalizi ya awali ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha tano na vyuo vya Serikali mwaka 2024.
Amesema Serikali imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye fomu za uchaguzi wa wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni.
Kwa mujibu wa Mchengerwa mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2024 na mitaala ya elimu kwa kidato cha tano yameanza kutekelezwa ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa tahasusi mpya 49 kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia 65.
Amefafanua kuwa tahasusi mpya zitakazoanza kutekelezwa Julai zipo katika makundi saba ambayo ni Sayansi ya Jamii, Lugha, Masomo ya Biashara, Sayansi, Michezo, Sanaa na Elimu ya Dini.
“Kukamilika kwa zoezi hili kunatoa fursa kwa wanafunzi kufanya mabadiliko ya machaguo ya tahasusi na kozi kwa njia ya mtandao. Baada ya wanafunzi kufanya marekebisho kanzidata hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia nafasi za kidato cha tano na kozi mbalimbali katika vyuo vya kati na vya elimu ya ufundi kwa kuzingatia sifa za ufaulu na machaguo yao,” amesema Mchengerwa.
Waziri huyo amesema zoezi hilo litatoa fursa zaidi ya wanafunzi kuongeza machaguo na kufanya machaguo mapya ya tahahusi na kozi.
Amesema zoezi hilo lililoanza Machi 19 litahitihimishwa Machi 30,2024 na kuwataka wazazi na walezi kushiriki kwa kushauriana na watoto wao katika kufanya machaguo sahihi kulingana na ufaulu wao.
Na Nora Damian, The Page