MAKONDA AONDOLEWA UKATIBU UENEZI AKIHUDUMU KWA MIEZI MITANO
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Na Mwandishi Wetu, The Page
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya viongozi wa wizara na mikoa ambapo amemteua aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Oktoba 23,2023 Makonda aliteuliwa kushika wadhifa huo wa uenezi akimrithi Sophia Mjema ambaye aliteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa masuala ya wanawake na makundi maalumu.
Taarifa ya mabadiliko hayo imetolea leo Machi 31,2024 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Kulingana na taarifa hiyo Makonda anachukua nafasi ya John Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wengine walioteuliwa ni Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi Ofisiy a Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) akimrithi Profesa Joyce Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Vilevile wamo Kanali Evans Mtambi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Said Mtanda ambaye amehamishiwa Mkoa wa Mwanza kumrithi Amos Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Katika orodha hiyo pia Zainab Katimba ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) huku Daniel Sillo akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua nafasi ya Jumanne Sagini ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Waziri.
Rais Samia pia amemhamisha Maryprisca Mahundi kutoka Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuchukua nafasi ya Kundo Mathew ambaye amehamishiwa Wizara ya Maji.
Wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Fakii Lulandala (Mkuu wa Wilaya ya Simanjro), Gilbert Kalima (Mkuu wa Wilaya ya Mkinga), Mhandisi Cyrpian Luhemeja (Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira), Mary Maganga (Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Aidha Dk. Edwin Mhede ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Agnes Meena ambaye amehamishiwa Wizara ya Maji.

Dk. Suleiman Serera ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uramaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Nicholaus Mkapa ambaye amehamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Rais Samia pia amemteua Selestine Kakele kuwa Balozi na Dk. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
Viongozi hao wataapishwa Aprili 4,2024 Ikulu, Dar es Salaam.