MAAMBUKIZI MAPYA MATENDE, MABUSHA YABAKI HALMASHAURI 7
Ugonjwa wa matende na mabusha huenezwa na mbu na husababisha kuvimba kwa viungo vya mwili hasa miguu.
Na Nora Damian, The Page
Serikali imesema maambukizi mapya ya ugonjwa wa matende na mabusha yamepungua kutoka halmashauri 119 hadi kufikia halmashauri saba mwaka 2024.
Mafanikio hayo yamechangiwa na kampeni za utoaji elimu na umezaji kingatiba za ugonjwa huo zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Akizungumza leo Machi 12,2024 na Waandishi wa habari Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema walifanya tathmini kati ya Machi hadi Agosti 2023 na Februari 2024.
“Ugonjwa wa matende na mabusha ni miongoni mwa changamoto kubwa za kiafya zinazowaathiri wananchi, tukiangalia miaka 10 au 15 iliyopita tunajivunia tumepunguza maambukizi mapya,” amesema Ummy.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizofikiwa kutokomeza ugonjwa wa matende na mabusha nchini.
Amezitaja halmashauri ambazo bado zina maambukizi mapya kuwa ni Pangani, Mafia, Kinondoni, Kilwa, Lindi Manispaa, Mtama na Mtwara Mikindani.
Aidha amesema Kigamboni na Ubungo hazina maambukizi mapya kwa kipindi cha miaka sita baada ya kusitisha umezaji wa kingatiba hatua iliyowezesha watu milioni 3.7 kuokolewa katika hatari ya kupata maambukizi mapya jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo amesema kata 10 za Halmashauri ya Kinondoni bado zina maambukizi mapya kwa kiwango cha asilimia 2.5. ambazo ni Tandale, Kijitonyama, Mwananyama, Kigogo, Mzimuni, Magomeni, Ndungumi, Hananasif, Kinondoni na Makumbusho.
“Tunaweza kutokomeza maambukizi mapya endapo tutaweka mkazo katika kata 10 zilizobaki, tunasitisha rasmi kampeni za umezaji wa kingatiba za mabusha na matende katika maeneo ya Dar es Salaam ambayo hayana maambukizi,” amesema.
Waziri huyo amewataka wananchi waendelee kujikinga na maambukizi mapya ikiwemo kutokomeza mazalia ya mbu na kushiriki katika kampeni zitakazoendeshwa za kingatiba na kuwahakikishia kuwa dawa hizo ni salama.
Pia amewataka watu wenye magonjwa hayo kujitokeza kupata huduma za upasuaji ambazo zinagharamiwa na Serikali.

Aidha amesema Desemba 2023 kando ya mkutano wa mazingira uliofanyika jijini Dubai pia walijadili kuhusu kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo Rais Samia aliahidi kuwekeza Dola za Marekani milioni 3 katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024 ili kuyatokomeza.
Naye Mratibu Udhibiti wa Ugonjwa wa Matende na Mabusha Wizara ya Afya, Dk. Faraja Lyamuya, amesema sababu zinazochangia maambukizi mapya katika baadhi ya maeneo ni jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha na kuhamahama hatua inayosababisha kutoshiriki kikamilifu katika umezaji wa kingatiba.
Kuhusu maambukizi mapya kuwa maeneo ya Pwani zaidi amesema ni kwa sababu ya hali ya hewa na mazingira ambayo huruhusu mazalia ya mbu na kwamba mazalia yenye mbu wengi ndiyo yalionekana kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi.
Tathmini inaonyesha kambi ya mwisho ya upasuaji wa mabusha na matende ilifanyika mwaka 2023 na kuvuka lengo la kufanya upasuaji kwa zaidi ya watu 1,100.