BEI YA SUKARI SH 2,700
Na Mwandishi Wetu, The Page
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza bei elekezi ya sukari ili kupunguza gharama za maisha katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
Mfungo wa Ramadhani unaanza leo Machi 12,2024.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban, amesema kilo moja ya sukari itauzwa kwa Sh 2,650 kwa Unguja na Sh 2,700 kwa Pemba.
Awali bei ya rejareja ya sukari ilikuwa Sh 3,200.
