WANANCHI KIJIJINI MAKAO WAFURAHIA HUDUMA YA MAJI
Na Mwandishi Wetu, Meatu
Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Maji imefanikisha huduma ya majisafi kwa asilimia 100 kwa wananchi waishio kijijini Makao.
Inawezekana wapo wanaojua jina hilo linapotamkwa wanaenda moja kwa moja Bara la Asia, katika nchi ya China kwa maana ya Macau, iliyokuwa koloni la Ureno.
La hasha. Hii Makao ipo Kata ya Mwangudo Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Tanzania, na eneo hilo lina hifadhi ambayo ni kiungo kati ya Hifadhi ya Maswa na ile ya Serengeti.
Eneo hilo ni muhimu kwa sababu pamoja na maisha ya kila siku ya mwanadamu na kazi zake ni ushoroba wa wanyamapori katika hifadhi inazopakana nazo.
Makala haya yanazungumzia huduma ya majisafi kwa wananchi katika eneo hilo ambalo kwa kipimo cha jiografia yake imezungukwa na hifadhi za wanyamapori.
Ukweli unabaki kuwa msimu wa kiangazi endapo huduma ya maji isingekuwepo, wakazi wa eneo hilo ingewalizimu kwenda katika mabonde ya mito au chemichemi ambako wanyama mbalimbali nao hufuata maji, hivyo kuleta sintofahamu ya binadamu na wanyama katika kupata maji.
Meneja wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Meatu, Mhandisi Neliko Emmanuel, anasema kazi kubwa imefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita na pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikia wananchi katika eneo hilo, kwa huduma ya uhakika ya majisafi ya bombani.
Taswira ya Kijiji cha Makao, Meatu mkoani Simiyu ikionyesha mandhari ya mazingira ya mashamba na shughuli za kilimo zinazoendelea na mitaa iliyopangika, ikiwa imezungukwa na misitu iliyotunzwa vizuri.
“Mwanzo kijijini hapa hatukuwa na maji ya bomba kabisa jambo ambalo halikuwa salama kwa wananchi, kama unavyoona pande zote tumezungukwa na hifadhi. Serikali imeondoa wasiwasi huo kwa wananchi na kuhakikisha maji yanafika katika makazi na vituo vya umma vya kuchotea maji," anasema.
Mradi huo wa maji umefanikishwa na Serikali kupitia Programu ya Lipa kwa Matokeo (PforR) ambayo imepigiwa mfano kati ya nchi zaidi ya 50 duniani na kuifanya Tanzania kuwa kinara katika utekelezaji wake na kufikisha huduma ya maji katika jamii. Thamani ya program hiyo ni zaidi ya Sh milioni 815.
Mhandisi Neliko anasema kutokana na mazingira ya Makao kuzungukwa na hifadhi, suala la ushirikishwaji wa askari wa wanyamapori limekuwa zuri na la mfano kwa maeneo mengine yenye mazingira kama hayo.
Anasema mradi huo unatumia nishati ya jua (solar) hivyo huduma inapatikana saa 24 na kwa gharama nafuu kwa huduma na uendeshaji.
Anasema katika kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wadau wote, serikali imefikisha huduma ya maji katika kambi ndani ya hifadhi ili kutoa huduma kwa wateja na watumishi wote katika eneo hilo.
Benjamin Ruben, ambaye ni Katibu wa Chombo cha Watumia Maji katika eneo hilo anasema kazi ya kuongeza vituo vya umma vya kuchotea maji inaendelea na wananchi wanaendelea kunufaika na huduma ya maji. Hivi sasa mradi huo una jumla ya vituo nane vya kutoa huduma kwa umma na wananchi wanaweza kuunganishwa nyumbani.
Serikali kupitia mradi huo imehakikisha huduma ya maji inafika katika sehemu zinazotoa huduma kwa umma, ikiwamo Shule ya Msingi Makao na Shule ya Sekondari Makao hatua ambayo imeleta utulivu kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo na zahanati.
Vijijini na mijini kwa ujumla huduma ya maji ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na mabadiliko makubwa ya uchumi. Dira ya Maendeleo ya 2025 inatambua hilo kwamba maji ni kipaumbele katika kuleta hali bora katika maisha ya wananchi.
Kuimarisha huduma ya maji kwa jamii inaleta uhakika wa mafanikio ya kijamii na uchumi ikiwamo uwekezaji mkubwa.
Diwani wa Kata ya Mwangudo, Anthony Phillipo, akiongea kijijini Makao anatoa pongezi kwa Serikali na Rais Samia kwa kutoa majibu ya changamoto ya majisafi katika Kijiji cha Makao.
“Maji ilikuwa ni tatizo, mradi huu umekuwa ni mwarobaini wa huduma ya maji hapa Makao na tunawaombea viongozi wote wapate nguvu zaidi kwani wamegusa maisha yetu,” anasema Diwani Phillipo.
Anaongeza hivi sasa wananchi hawachimbi tena katika mabonde kutafuta maji hivyo shida ya kukimbizana na wanyama kutafuta maji kwa matumizi mbalimbali imefika mwisho.
Mkazi wa Kijiji cha Makao, Salome Mnyampanda, kuhusu huduma ya maji anasema sasa kuna amani baada ya kupata huduma ya majisafi kijijini hapo.
Anasema kila mwanakijiji anajihudumia mweyewe kwa muda anaotaka bila kuwa na changamoto yoyote hata ambao umri umeenda kama yeye hawapati tatizo kupata maji.
“Sisi kina mama wa Makao tunamshukuru Rais Samia kwa katuletea amani na tunamkaribisha hapa aone huduma ilivyo bora," anasema Mnyampanda.
Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa mwaka 2022 bado kulikuwa na idadi kubwa ya watu wasiopata huduma ya maji wapatao milioni 226.
Kupitia programu ya Lipa kwa Matokeo (PforR) Wizara ya Maji imetekeleza zaidi ya miradi ya maji 1,500 ambayo imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali na kusaidia kuongeza thamani ya bidhaa nyingine katika soko.
Ikumbukwe Serikali imepanga kufikia lengo la upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa asilimia 85 vijijini na mijini asilimia 95.
Kwa mapinduzi yanayofanyika katika miradi ya sekta ya maji hadi Desemba 2022 hali ya upatikanaji wa huduma ya maji hapa nchini ilikuwa asilimia 88 mijini na vijijini asilimia 77, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maji.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dk. Victoria Kwakwa, Novemba 2023 akiwa katika mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika unaohusu masuala ya upatikanaji wa majisafi na salama na usafi wa mazingira nchini Ethiopia aliipongeza Tanzania kwa kutekeleza kwa ubora na viwango Programu ya PforR na kuwa kinara wa nchi nyingine duniani zaidi ya 50 zinazotekeleza programu hiyo.
Dk. Kwakwa katika mkutano huo aliitaka Tanzania kutoa uzoefu wa mafanikio yake kwa nchi zaidi ya 23 za Mashariki na Kusini mwa Afrika ambazo zilishiriki mkutano huo.
Takwimu za Wizara ya Maji zinaonyesha hadi Aprili 2023, vituo 136 vya kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji vilikuwa vimekarabatiwa na vingine sita kujengwa, vibali vipya 1,554 vya matumizi ya maji na vibali 630 vya kuchimba visima vya maji kutolewa.
Watafiti wa masuala ya maji wanabashiri kuwa yapo masuala ambayo yanaweza kuathiri huduma hiyo kwa siku zijazo ikiwamo kuongezeka kwa idadi ya watu na mgawanyo wao, matumizi ya teknolojia na uchumi kwa kuongezeka uchafuzi wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi na hali ya mazingira kama vile mvua chache na kipindi kirefu cha joto na matumizi kupita kiasi cha maji yenyewe. Kukosekana kwa usimamizi wa rasilimali za maji nako kunachangia kuathiri huduma hiyo katika maeneo mbalimbali duniani.
Matumizi ya maji duniani yanatabiriwa kuongeza kwa asilimia 20 hadi 50 katika kipindi cha miaka 20 ijayo kutoka kiasi kinachotumika hivi sasa kwa sababu ikiwamo kuongezeka kwa namba ya viwanda na matumizi ya jamii.
Esha Zaveri wa Benki ya Dunia anasema asilimia 60 ya idadi ya watu duniani hupata janga la uhaba wa maji kwa uchache kati ya misimu ya hali ya hewa ya mwaka mmoja. Miongoni mwa vichochezi vya janga hilo ni kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji.
Tanzania ni tajiri wa rasilimali za maji. Atlasi ya Rasilimali za Maji (2019) inaonyesha rasilimali za maji zilizopo nchini ni wastani wa mita za ujazo bilioni 126 kwa mwaka ambapo juu ya ardhi ni mita za ujazo bilioni 105 na ardhini ni mita za ujazo bilioni 21.
Hivyo, kiasi cha maji kilichopo kwa kila mtu kwa mwaka ni wastani wa mita za ujazo 2,105. Hii ni kwa idadi ya watu milioni 59.8 waishio Tanzania Bara kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022. Kiwango kinachotajwa ni juu ya wastani wa mita za ujazo 1,700 kwa mtu kwa mwaka kinachokubalika kimataifa.
Takwimu zinaonesha inatarajiwa kufikia kiwango cha wastani wa mita za ujazo 1,700 kwa mwaka kwa mtu ifikapo mwaka 2030. Pamoja na hayo, mahitaji ya maji nchini kwa sekta mbalimbali kwa mwaka 2022 yalikuwa ni wastani wa mita za ujazo bilioni 62 na yanatarajiwa kufikia mita za ujazo bilioni 75 mwaka 2030. Hivyo, upo wajibu wa kuendelea kuongeza msukumo katika utunzaji wa rasilimali za maji, kuongeza ufanisi katika matumizi ya maji pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji ikiwa ni pamoja ujenzi wa mabwawa.
Ni wazi kuwa wakati jamii ina uhitaji mkubwa wa huduma ya maji, suala la usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nalo ni muhimu kwa wanajamii wote popote pale walipo.
Usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji unahusisha tathmini na ufuatiliaji wa rasilimali za maji; kuhifadhi na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji; kugawa maji kwa sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji na kiasi cha maji kilichopo; na kuendeleza rasilimali za maji.