KESI KAMPUNI YA NDONDI, AZAM MEDIA KUSIKILIZWA KWA MAANDISHI
Wakili Wwinnie Kawandakamu wa Kampuni ya Uwakili ya ABC, anayeitetea Kampuni ya Ndondi ya Hall of Fame Boxing and Promotion
akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mahakama Kuu imepanga kusikiliza kwa njia ya maandishi kesi ya madai dhidi ya Kampuni ya Ndondi ya Hall of Fame Boxing and Promotion na Azam Media.
Katika kesi hiyo namba 100/2023 Kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion inadai fidia ya Sh bilioni 2 kwa madai kuwa Azam imerusha maudhui yake katika runinga kinyume cha makubaliano.
Oktoba 24,2023 kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo mbele ya Jaji A. Mbagwa ambaye amepanga isikilizwe kwa njia ya maandishi kuanzia Desemba 6,2023.
Katika kesi hiyo Kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion inawakilishwa na Wakili Wwinnie Kawandakamu wa Kampuni ya Uwakili ya ABC.
Inadaiwa kuwa Azam ilikiuka makubaliano ya kimkataba kwa kurusha maudhui kwenye kipindi yaliyohusu mapambano mawili.
Mapambano hayo ni kati ya bondia Hassan Mwakinyo na rais wa Ufilipino, Arnel Tinampay na Twaha Kiduku dhidi ya Dulla Mbabe. Azam inadaiwa kuyarusha bila ya kuwa na haki miliki ya maudhui hayo.

