DK KIJAJI AIELEKEZA BRELA KUWALEA WAFANYABIASHARA
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa kongamano la Brela na wadau wake lililofanyika Mlimani City, Dar es Salaam.
Na Nora Damian, Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji ameutaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kuwalea wafanyabiashara na kuwa wabunifu wa namna ya kuwahudumia ili kufikia malengo ya uanzishwaji wake.
Ametoa maelekezo hayo Oktoba 27,2023 wakati akifungua kongamano la kwanza la Brela na wadau wake lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Amesema tangu mwaka 2019 hadi Juni, 2023 Serikali imeendelea kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira bora ya biashara na kuondoa tozo na kodi mbalimbali zaidi ya 374 zilizosumbua wafanyabiashara ambapo imefikia zaidi ya asilimia 75 ya dhamira yake.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa, wakifuatilia kongamano la Brela na wadau wake lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kukabidhi uchumi wa taifa kwa sekta binafsi na amefungua mipaka yote, hivyo taasisi inayoshughulikia sekta binafsi ni Brela kwa kuwa uchumi wa nchi unakua kupitia ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara nchini.
“Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia Sheria ya Fedha jumla ya Sheria na Kanuni 13 na Sheria ya Fedha ya mwaka 2023 zimeweza kupunguza na kufuta tozo, ada na faini 67 ikiwa ni lengo la Serikali kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa bora zaidi.
"Hakuna uchumi wa nchi unaokua kama hakuna maendeleo katika sekta ya viwanda na ya biashara iliyo imara, ndiyo maana Serikali inahakikisha inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara ndani na nje ya Tanzania na taasisi za udhibiti hazitumii mamlaka zao kufungia biashara yoyote lengo ni kuhakikisha kuwa sekta ya biashara inalea uchumi wa nchi," amesema Dk. Kijaji.
Waziri huyo amesema wameweka dhamira ya kuboresha sera na sheria ili zisomane na mabadiliko ya uchumi na kwamba wanaangalia uwekezano wa kutoa leseni zote za biashara katika mfumo mmoja wa Brela kuliko kuwa na mifumo mingi inayotoa huduma za leseni.
"Hii itasaidia uratibu mzuri wa leseni za biashara na Serikali kuwa na kanzi data moja ya taarifa za biashara, tunawaomba mtupe ushirikiano katika hatua hii ili kuwahudumia kwa ufanisi mzuri," amesema.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo, Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, amesema wafanyabiashara wengi hukimbilia Brela ili kupata huduma za mikopo kutoka taasisi za fedha na kupata zabuni lakini wengi hawaelewi tafsiri za kisheria za kampuni, hivyo ameushauri wakala huo kuzitafsiri kwa lugha nyepesi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, akiangalia bidhaa za washiriki wa Maonesho ya Huduma za Brela na Wadau Wake yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa, amesema wanatambua kuna sheria nyingi ambazo zimepitwa na wakati na wapo kwenye hatua za maboresho ya sheria hizo.

Amezitaja baadhi sheria hizo kuwa ni Sheria ya Viwanda ya mwaka 1967, Sheria ya Hataza ya Mwaka 1987, Sheria ya Miliki Bunifu ya Mwaka 1986 na Sheria ya Kampuni ya Mwaka 2002 ili ziendane na mabadiliko ya kiteknolojia na ukuaji wa sekta ya biashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Brela, Profesa Neema Mori, amesema wamepokea maoni yote ya wadau na kuwahakikishia kuwa watasimamia taasisi hiyo ili kuleta urahisi wa matumizi ya mifumo kuwa kidigitali na kusimamia michakato ya kuwepo kwa sera na maboresho ya sheria mbalimbali.