UWT KARIAKOO WAIUNGA MKONO SERIKALI SEKTA YA ELIMU


Na Pilly Kigome


Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Kata ya Kariakoo umeendelea kuiunga mkono Serikali katika sekta ya elimu kwa kugawa vifaa vya mitihani katika shule za msingi.

Hatua hiyo pia inalenga kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika utekelezaji wa sera zake ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya UWT.

Hayo yamesemwa Oktoba 27,2023 na Katibu Mkuu UWT Kata ya Kariakoo, Aisha Ausi, katika Shule ya Msingi Lumumba jijini Dar es Salaam.

Ausi ameuambia mtandao huuu kuwa wameona waunge mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan anazozifanya hususani katika sekta ya elimu nchini.



Amesema wanaiunga mkono shule hiyo kwa kuwapelekea vifaa vya elimu ili wanafunzi waweze kufanya mitihani yao mwishoni mwa mwaka kwa urahisi pasipo uwepo wa michango ya uchangishaji.

“Tumeleta vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nne, ikiwemo boksi za karatasi, 'expanding file', 'office pini' na vifaa vingine,” amesema Ausi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmanuel Herlman, ameushukuru umoja huo kwa kuichagua shule hiyo na kuwaletea vifaa ambavyo wanaamini vitawasaidia katika misimu michache ya kipindi cha mitihani.

Hata hivyo amesema shuleni hapo wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa viwanja vya michezo ya watoto.

Amesema changamoto hiyo inasababisha kuwe na uharibifu na ukarabati wa mara kwa mara wa madawati kutokana na watoto kucheza juu ya madawati.

Powered by Blogger.