JOKATE ATEULIWA KATIBU MKUU UWT
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), Jokate Mwegelo.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapindunzi (CCM) imemteua Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT).
Kabla ya uteuzi huo Jokate alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.
Kamati Kuu imekutana leo Oktoba 1,2023 jijini Dar es Salaam katika kikao chake maalumu na kufanya uteuzi huo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, imeeleza kuwa Kamati Kuu imemteua pia Fakii Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe.
Mwingine aliyeteuliwa ni Hamad Khamis Hamad kugombea uwakilishi katika Jimbo la Matembwe.
Na Nora Damian

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Fakii Lulandala.