SAMIA AMTEUA MOBHARE MATINYI MSEMAJI MKUU WA SERIKALI
Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo Matinyi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Oktoba 1,2023 imeeleza uteuzi huo unaanza mara moja.
Nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya Gerson Msigwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
