RAIS SAMIA APIGIA CHAPUO VISION 2030
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman, akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Dira ya Sekta ya Madini (Vision 2030) itamaliza changamoto za muda mrefu kwa wachimbaji wadogo za kukosekana kwa taarifa za kuaminika za maeneo yenye rasilimali hiyo.
Dira hiyo ‘Madini ni Maisha na Utajiri’ imelenga kuhakikisha hadi kufikia 2030 utafiti wa madini kwa njia za jiofizikia uwe umefanyika nchini wa zaidi ya asilimia 50.
Katika hotuba yake iliyosomwa leo Septemba 30,2023 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman, wakati wa kufunga Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita, amesema utafiti huo utasaidia kujua maeneo yenye madini.
“Serikali inaendelea kuhakikisha wachimbaji wa madini wanapata masoko ya uhakika na itaendelea kuwawezesha wawekezaji wadogo wa sekta hii kwa kuwaunganisha na taasisi za fedha,” amesema Rais Samia.
Amesema ili sekta ya madini iweze kuongeza mchango wale lazima ifungamanishwe na sekta nyingine kuwezesha taifa kupata maendeleo kwa haraka na upatikanaji wa ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Mbunge wa Jimbo la Busanda, Tumaini Magesa, ameishauri Serikali kuboresha miundombinu ya barabara ikiwemo ya Geita – Ulyankulu – Kahama ili kuwapunguzia gharama za uendeshaji wachimbaji na kuwawezesha kupata faida.
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu, amesema mahitaji makubwa ya wachimbaji ni teknolojia, mitaji na masoko ili kutengeneza ajira zaidi kwa Watanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amesema mkoa huo ni wazalishaji wakubwa wa dhahabu ambapo imezalisha kilo 47,000 na kati ya hizo 36,000 zimezalishwa na wachimbaji wakubwa na 11,000 wachimbaji wadogo.
“Miaka ya nyuma uzalishaji haukuwa hivi, Rais Samia ameipa msukumo sekta ya madini katika nchi yetu,” amesema Shigela.
Kwa mujibu wa Shigela leseni 2,411 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo na zingine 300 watakabidhiwa kuwawezesha kuchimba kisasa.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema wanaamini ifikapo mwaka 2025 mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa utafikia asilimia 10 kama inavyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.
Kwa mujibu wa Mavunde, sekta ya madini ndiyo inaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni ambapo kwa mwaka 2022/2023 iliingiza zaidi ya Dola bilioni 3.3 sawa na zaidi ya Sh trilioni 7.
“Vision 2030 tunakusudia kufanya utafiti ili kupata taarifa za miamba na madini kwa sababu wachimbaji wanachimba kwa kubahatisha, wanapoteza mitaji na nguvu zao…tutarusha ndege, drones na helikopta na kupiga picha ili kupata taarifa za awali,” amesema Mavunde.
Na Nora Damian, Geita

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Ametoa wito kwa Benki Kuu ya Tanzania iendelee kununua dhahabu ili nchi iweze kuwa na akiba ya kutosha.
Mbunge wa Jimbo la Busanda, Tumaini Magesa, ameishauri Serikali kuboresha miundombinu ya barabara ikiwemo ya Geita – Ulyankulu – Kahama ili kuwapunguzia gharama za uendeshaji wachimbaji na kuwawezesha kupata faida.
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu, amesema mahitaji makubwa ya wachimbaji ni teknolojia, mitaji na masoko ili kutengeneza ajira zaidi kwa Watanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amesema mkoa huo ni wazalishaji wakubwa wa dhahabu ambapo imezalisha kilo 47,000 na kati ya hizo 36,000 zimezalishwa na wachimbaji wakubwa na 11,000 wachimbaji wadogo.
“Miaka ya nyuma uzalishaji haukuwa hivi, Rais Samia ameipa msukumo sekta ya madini katika nchi yetu,” amesema Shigela.
Kwa mujibu wa Shigela leseni 2,411 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo na zingine 300 watakabidhiwa kuwawezesha kuchimba kisasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman,
akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa GGML,Terry Strong, wakati wa kufunga Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa GGML,Terry Strong, wakati wa kufunga Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema wanaamini ifikapo mwaka 2025 mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa utafikia asilimia 10 kama inavyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.
Kwa mujibu wa Mavunde, sekta ya madini ndiyo inaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni ambapo kwa mwaka 2022/2023 iliingiza zaidi ya Dola bilioni 3.3 sawa na zaidi ya Sh trilioni 7.
“Vision 2030 tunakusudia kufanya utafiti ili kupata taarifa za miamba na madini kwa sababu wachimbaji wanachimba kwa kubahatisha, wanapoteza mitaji na nguvu zao…tutarusha ndege, drones na helikopta na kupiga picha ili kupata taarifa za awali,” amesema Mavunde.
Katika maonesho hayo Kampuni ya GGML ilipewa tuzo kutambua mchango wake ambapo imedhamini maonesho hayo kwa gharama ya Sh milioni 150.