SOTTA MINING YALIPA FIDIA SH BILIONI 15
Banda la Kampuni ya Sotta Mining katika Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Zaidi ya Sh bilioni 15.2 zimelipwa kwa wakazi 630 wa eneo la Nyanzaga Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kupisha uzalishaji madini utakaofanywa na Kampuni ya Sotta Mining (SMCL).
Kampuni hiyo inamiliki mgodi wa Nyanzaga wenye hisa ya asilimia 84 na Serikali ikiwa na hisa asilimia 16.
Akizungumza leo Septemba 30,2023 Mkuu wa Kampuni hiyo, Isaac Lupokela, amesema wanatarajia kuanza uzalishaji mwaka 2025.
“Hivi sasa tuko kwenye zoezi la kuwahamisha wakazi ambao wanaguswa na mradi na tayari tumeshawalipa fidia, matarajio yetu tunategemea kuanza uzalishaji mwaka 2025 baada ya ujenzi wa mgodi kukamilika,” amesema Lupokela.
Amesema walipata leseni ya uchimbaji Desemba 2021 na wanatarajia kuzalisha wakia 240,000 kwa mwaka.
Kampuni hiyo inajenga mradi wa dhahabu wa Nyanzaga katika Vijiji vya Sotta na Nyabila Kata ya Igaula Wilaya ya Sengerema.
Na Nora Damian, Geita