WANAWAKE GEITA WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA MATUMIZI NISHATI MBADALA
Mwenyekiti wa Wanawake na Samia katika Mkoa wa Geita, Adelina Kabakama, akizungumza kwenye Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Katika jitihada za kupunguza ukataji miti na uharibifu wa mazingira wanawake mkoani Geita wamehamasika na kuanza kutumia nishati mbadala.
Tathmini iliyofanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) inaonyesha hekta 46,960 ambayo ni asilimia 26 ya ardhi huharibiwa kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.
Akizungumza Septemba 22,2023 Mwenyekiti wa Wanawake na Samia katika Mkoa wa Geita, Adelina Kabakama, amesema wanahamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza ukataji miti.
Kabakama alikuwa akizungumza na Mtandao wa The Page kwenye Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA mkoani Geita ambapo wana banda lao.
Amesema kikundi hicho kiliundwa kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kupinga ukatili wa kijinsia, kuinua uchumi wa kinamama na kutunza mazingira.
“Katika kutunza mazingira tumeunganishwa na Stamico (Shirika la Madini la Taifa) ambao wametuwezesha katika upandaji miti na sasa wanataka kutupatia uwakala wa kuuza mkaa mbadala na kuhakikisha wananchi wanaupata kwa bei nafuu.
“Kilo moja inauzwa kwa shilingi elfu moja ambayo unaweza ukapika chakula kikaiva na wakati mwingine mkaa ukabaki,” amesema Kabakama.
Amesema kikundi hicho ambacho kimewaunganisha wajasiriamali wadogo, wafanyakazi na viongozi wa Serikali tayari kina ushirika wa kuuza nafaka mbalimbali ambapo wameanza na mchele ili kujiendeleza kiuchumi.
“Tunapambana tumiliki kiwanda cha kuchakata mchele, unga tuuze ndani na nje ya nchi ili uchumi wetu kinamama uzidi kukua,” amesema.

Mwenyekiti wa Wanawake na Samia katika Mkoa wa Geita, Adelina Kabakama, akionyesha mkaa mbadala kwenye Maonesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Kuhusu ukatili wa kijinsia amesema wamekuwa wakitoa elimu katika shule mbalimbali na kufanya midahalo na makongamano kwenye jamii.
“Umaskini ndio unaochangia ukatili, mama kama hana kipato chochote anakuwa ni tegemezi kwa baba. Familia inapokuwa na uchumi imara ukatili wa kijinsia hautakuwepo kwa sababu kila mmoja atatimiza wajibu,” amesema.
Amesema wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada mbalimbali anazozifanya za kuwaletea Watanzania maendeleo.
“Yale yote ambayo mama anayafanya tunayaeleza kwenye jamii, tunaona jinsi mama alivyojenga hospitali, shule na mambo mengine mengi. Wengi wanamwelewa mama na tutaendelea kumuunga mkono kwa sababu tunaona jinsi anavyotupatia fursa,” amesema Kabakama.